Psalms 37:3-8


3 aMtumaini Bwana na utende yaliyo mema;
Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama.

4 bJifurahishe katika Bwana
naye atakupa haja za moyo wako.


5 cMkabidhi Bwana njia yako,
mtumaini yeye, naye atatenda hili:

6 dYeye atafanya haki yako ing’ae kama mapambazuko,
na hukumu ya shauri lako kama jua la adhuhuri.


7 eTulia mbele za Bwana
na umngojee kwa uvumilivu;
usisumbuke watu wanapofanikiwa katika njia zao,
wanapotekeleza mipango yao miovu.


8 fEpuka hasira na uache ghadhabu,
usihangaike: itakuongoza tu kutenda uovu.
Copyright information for SwhKC